Katika kutekeleza majukumu ya kazi nimeweza kuona mambo mengi sana na hasa changamoto za kisiasa ndipo nikagundua kuwa:--------
1:Kuna baadhi ya viongozi walioko Bungeni hawazijui sheria pamoja na kuwa wanazitunga na kizipitisha wao wenyewe
2:Kuna baadhi ya Viongozi hawataki sheria ifanye kazi yake badala yake wanaangalia kura zaidi kuliko Uhifadhi zaidi hata kama wapiga kura wao wamevunja sheria wamevunja hapo utakuta anapikga kelele pasipo kujua wapigakura wake wamevunja sheria pasipo kuwa na mafanikio
3:Elimu ya UHIFADHI hapo katika jamii zinazozizunguka uhifadhi
Zetu
4:Baadhi ya Viongozi ni waoga Katika kutekeleza majukumu yao na inapofikia sehemu ya kutekeleza sheria .
5:Baadhi ya Viongozi hawana msaada na hasa kwenye matatizo yaani utakuta kitu kilikuwa cha kiofisi utashangaa umebaki peke yako hakuna wa kukusaidia huoni Hata kiongozi mmoja hadi ujinasue wewe mwenyewe hivyo utakuta mtu anafanya kazi kwa kuangalia upande wake kuliko kufanya kazi ujasiri anakuwa hana
6:Lakini pia kuna viongozi ni wafuatiliaji na wanaijua sheria ya Wanyama Pori hadi unajihisi raha Hata kama uko kwenye majukumu yako ya kutekeleza sheria
Uhifadhi ni muhimu sana kwa kizazi cha sasa na kijacho kutekeleza sheria yetu iliyotungwa na kupitishwa pamoja na kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Uhifadhi wetu uwe endelevu na uweze kiongozi serial mapato na hayo mapato yainufaishe jamii nzima ya Tanzania sio iharibiwe na watu wachache na sisi wahifadhi tupo maana Mimi naamini watanzania wote ni wahifadhi.
By Uhifadhi.