Friday, December 4, 2015

TARANGIRE NATIONAL PARK

Tanzania inavivutio vingi sana hiki ni kichuguu chenye zaidi ya mita tano kinapatikana Tarangire National Parks Tujengeni tabia ya kuzitembelea hifadhi zetu tujionee vivutio vilivyopo nchini kwetu maana vingine ni maajabu

Published with Photo Blogger for Windows Phone.

BAD NEWS TO WILDLIFE WARDEN

HABARI MBAYA KWA WAHIFADHI Wanyama aina ya Nyati nane (8) wamegongongwa na gari aina ya Fuso katika hifadhi ya Taifa Mikumi leo Hii ni mbaya sana maana barabara imepita hifadhini na sioni sababu ya hiyo barabara kupitishwa humo maana kila siku kila mwaka wanyama wanagongwa lakini uongozi wa hifadhi hiyo sioni kama unashughulikia hii mambo. kwa nini hii barabara isitolewe hifadhini ipite kwingine hii mamlaka husika ziwajibike hatuwezi kuwa tunapoteza wanyama wengi bila sababu za msingi Ni hayo tu

Published with Photo Blogger for Windows Phone.

Tuesday, December 1, 2015

MKUU WA MKOA WA KAGERA

Huyu mkuu wa Mkoa wa Kagera ameukosha sana sana moyo wangu kwa hili tamko kwa wafugaji waliovamia mapori ya Burigi Biharamuro na Kimisi kutoa mifugo hifashini uhifadhi uchukue nafasi yake asante sana ‪#‎HapaKaziTu‬ Huyu mkuu wa Mkoa wa Kagera ameukosha sana sana moyo wangu kwa hili tamko kwa wafugaji waliovamia mapori ya Burigi Biharamuro na Kimisi kutoa mifugo hifashini uhifadhi uchukue nafasi yake asante sana ‪#‎HapaKaziTu‬

Published with Photo Blogger for Windows Phone.

TEMBO

TEMBO Tembo ni kati ya wanyama wanaoelekea kupotea kulingana kupungua kwao kwa kasi zaidi kutokana na ukweli kwamba anawindwa zaidi kwa sababu ya meno au pembe za ndovu alizonazo. Hivyo yatupasa kumtunza sana maana tusipofanya hivyo atapotea na vizazi vijavyo vitakutakuta historia tu lakini havitawaona hao tembo. Ili tufanikiwe lazima tushirikiane kwa pamoja wahifadhi na wananchi kuwalinda hawa wanyama ADIMU tuliopewa na mwenyezi Mungu. Inasikitisha na ni ukatili uliopitiliza kumuua mnyama mkubwa kama tembo na lengo ni kutoa ndovu tu Pia mahakama zitusaidie kuwatia hatiani Majangili tunaowakamata kwa kuhatarisha maisha yetu ili kumkamata jangili anayejihusisha na ujangili wa meno ya tembo. Huwa inauma sana kumkamata jangili WA aina yoyote halafu baada ya siku unauona yuko mtaani sheria zitumike sasa ili uhifadhi wetu uwe endelevu kwa manufaa ya taifa letu

Published with Photo Blogger for Windows Phone.