Tuesday, December 1, 2015

TEMBO

TEMBO Tembo ni kati ya wanyama wanaoelekea kupotea kulingana kupungua kwao kwa kasi zaidi kutokana na ukweli kwamba anawindwa zaidi kwa sababu ya meno au pembe za ndovu alizonazo. Hivyo yatupasa kumtunza sana maana tusipofanya hivyo atapotea na vizazi vijavyo vitakutakuta historia tu lakini havitawaona hao tembo. Ili tufanikiwe lazima tushirikiane kwa pamoja wahifadhi na wananchi kuwalinda hawa wanyama ADIMU tuliopewa na mwenyezi Mungu. Inasikitisha na ni ukatili uliopitiliza kumuua mnyama mkubwa kama tembo na lengo ni kutoa ndovu tu Pia mahakama zitusaidie kuwatia hatiani Majangili tunaowakamata kwa kuhatarisha maisha yetu ili kumkamata jangili anayejihusisha na ujangili wa meno ya tembo. Huwa inauma sana kumkamata jangili WA aina yoyote halafu baada ya siku unauona yuko mtaani sheria zitumike sasa ili uhifadhi wetu uwe endelevu kwa manufaa ya taifa letu

Published with Photo Blogger for Windows Phone.

No comments:

Post a Comment